Je, alete Takbiyr nyingine anayesimama kukamilisha Rak´ah ya nne?

Swali: Je, mtu anapaswa kuleta Takbiyr kwa Rak´ah aliyokosa ikiwa ametoa salamu baada ya kuswali Rak´ah tatu badala ya nne, kisha akasimama kukamilisha Rak´ah nyingine?

Jibu: Halina msingi. Tayari ameshaleta Takbiyr alipoinuka kutoka sijda ya pili. Katika hali hiyo atasimama kwa nia ya kuendelea na swalah na kuikamilisha Rak´ah iliyokosekana, bila haja ya takbira nyingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24894/اذا-سلم-عن-ثلاث-ثم-اتى-بالفاىتة-هل-يكبر-لها
  • Imechapishwa: 27/12/2024