Swali: al-Qardhwaawiy anasema msingi ni kwamba hata ´Aqiydah ya Kiislamu ni lazima vilevile iafikiane na akili. Je, msingi huu ni sahihi? Ni vipi anaraddiwa ikiwa sio sahihi?

Jibu: Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala) amesema:

وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّـهِ

”Katika lolote lile mlilokhitilafiana basi hukumu yake ni kwa Allaah.” 42:10

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

“Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamwamini Allaah na siku ya Mwisho. Hivyo ni njia bora na matokeo mazuri zaidi.” 04:59

Ni umiliaji wa Suufiyyah na Mu´tazilah. Wanachukua kibaya kutoka katika kila madhehebu. Je, kuna jengine lililowafanya Mu´tazilah kupotea kama sio kwa ajili ya kutanguliza matamanio mbele ya Qur-aan na Sunnah? Sisemi kama wanavyosema, kwamba wanachotaka ni kuitanguliza akili kabla ya Qur-aan na Sunnah. Kwa kuwa akili timamu haipingani na nukuu sahihi. Qardhwaawiy! Umepotea kama walivyopotea Mu´tazilah.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iskaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 96
  • Imechapishwa: 08/10/2016