Istikhaarah inaswaliwa wakati mtu anasitasita au baada ya kuamua?

Swali: Je, swalah ya Istikhaarah huswaliwa wakati mtu anasitasita kati ya mambo mawili au wakati ameshakusudia jambo moja?

Jibu: Swalah ya Istikhaarah huswaliwa wakati wa kutatanika. Ikiwa ameshakusudia jambo lakini ana shaka au anasitasita kati ya mambo mawili; amedhamiria safari lakini ana tashwishi, anataka kufunga ndoa na mwanamke lakini ana kusitasita au mfano wa hayo, basi ataswali  Rak´ah mbili kisha ataomba ushauri kutoka kwa Allaah kuhusu jambo lililomtatiza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31692/هل-تكون-الاستخارة-عند-العزم-على-امر-ام-التردد
  • Imechapishwa: 14/11/2025