Swali: Ni ipi hukumu ya msemo huu:

“Ninajua kuwa ISIS ni Khawaarij, lakini hata hivyo wanahukumu kwa Shari´ah.”?

Jibu: Huu ni uongo. Hawahukumu kwa Shari´ah. Lau wangekuwa wanahukumu kwa Shari´ah kweli basi wasingefanya waliyoyafanya; kufanya uasi kwa watawala na kuwakufurisha waislamu. Wana mambo tele yenye kwenda kinyume. Ambaye wamemhukumu kifo wanamuunguza kwa moto. Wameenda kinyume na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah amefaradhisha kufanya wema juu ya kila kitu; hivyo mnapoua uweni kwa uzuri na mnapochinja chinjeni kwa uzuri.”

Inatakiwa kuua kwa panga. Haya ndio ambayo hatimaye waislamu wamekubaliana kwayo.

ISIS ni Khawaarij. Jengine ni kwamba kitendo hichi kinaenda kinyume na maafikiano ya waislamu. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ametaja maafikiano juu ya kuwaua Khawaarij na Raafidhwah wakienda kinyume na mkusanyiko. Mapote haya mawili yameenda kinyume na mkusanyiko. Tahadhari ewe mwanangu na njia za vichochoro.

 

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/11097
  • Imechapishwa: 06/11/2016