Swali: Ni upi msimamo sahihi kwa yule mwenye kuwatuma watoto wake ´Iraaq au Syria ili kupigana vita pamoja na makundi kama ISIS na mfano wao?
Jibu: Bila ya shaka haya ni katika matendo mabaya. Anatakiwa kutahadhari na asiwatume watoto wake huko. ISIS imekuwa vipi? Imekulia wapi nchi hii? Je, nchi hii inahakikisha Tawhiyd na kuwakataza watu kuabudu makaburi? Hii ni fitina imedhihiri kwa watu katika miaka hii ya nyuma. Mwenye kufaidika nayo na kuiita nchi ya Kiislamu… Magharibi lengo lake ni kuuchafua Uislamu kwa majina kama haya. Eti inaitwa “nchi ya Kiislamu”. Nchi hii imekulia vipi? Makundi ´Iraaq, Syria na watu wamewazunguka na kusema kuwa hii ni nchi? Ni mkusanyiko haribifu usiokuwa na kheri yoyote.
  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=149597
  • Imechapishwa: 06/11/2016