Swali: Ni kipi kidhibiti juu ya nguo yenye kuvuka kongo mbili za miguu? Tumesikia baadhi ya watu wanasema kuwa haina neno endapo mtu atavaa bila ya kiburi.
Jibu: Isbaal ni haramu na ni dhambi kubwa:
“Chenye kuvuka kongo mbili za miguu ni Motoni.”[1]
Inajumuisha koti, suruwali, thawb, kikoi – vyote. Lakini adhabu inakuwa kubwa endapo mtu atafanya kwa kiburi. Hapo kunakuwa kumekusanyika Isbaal na kiburi.
[1] al-Bukhaariy (5787).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsirayat-12-07-1435-01_0.mp3
- Imechapishwa: 20/06/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Ni ipi hukumu kwa mwanaume kuvaa nguo yenye kuvuka kongo mbili za miguu pasi na kukusudia kiburi?
Swali: Ni ipi hukumu kwa mwanaume kuvaa nguo yenye kuvuka kongo mbili za miguu pasi na kukusudia kiburi? Jibu: Kuvaa nguo yenye kuvuka kongo mbili za miguu ni jambo la haramu na halijuzu. Ikiwa mtu anavaa kwa kiburi basi dhambi inakuwa kubwa zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:…
In "Isbaal - Nguo ya mwanamme yenye kuvuka kongo za miguu"
Isbaal ni haramu katika hali zote
Swali: Baadhi ya Hadiyth zinazokataza mwanaume kuvaa nguo chini kongo mbili za miguu zimekuja kwa njia isiyo na masharti na baadhi zimefungamanishwa na kiburi. Je, zile zisizo na masharti zitafasiriwa kwa mujibu wa zile zilizoachiwa? Jibu: Hapana, zile zisizo na masharti hazitafasiriwa kwa mujibu wa zile zilizoachiwa. Ni haramu kabisa…
In "Isbaal - Nguo ya mwanamme yenye kuvuka kongo za miguu"
Nguo inayovuka kongo mbili za miguu ni haramu katika hali zote
Swali: Je, kuvaa nguo inayovuka kongo mbili za miguu ni katika madhambi makubwa au maasi tu? Jibu: Kunakhofiwa kuwa katika madhambi makubwa. Hilo ni kutokana na kemeo linalosema: “Allaah hatomtazama siku ya Qiyaamah.” Kufanya kiburi ni katika madhambi makubwa. Tunamuomba Allaah usalama. Swali: Imaam an-Nawawiy anaona kuwa inachukiza tu ikiwa…
In "Isbaal - Nguo ya mwanamme yenye kuvuka kongo za miguu"