Swali: Baadhi ya Hadiyth zinazokataza mwanaume kuvaa nguo chini kongo mbili za miguu zimekuja kwa njia isiyo na masharti na baadhi zimefungamanishwa na kiburi. Je, zile zisizo na masharti zitafasiriwa kwa mujibu wa zile zilizoachiwa?

Jibu: Hapana, zile zisizo na masharti hazitafasiriwa kwa mujibu wa zile zilizoachiwa. Ni haramu kabisa katika kila hali.

Swali: Je, mikono mirefu ya kanzu ina hukumu hiyohiyo?

Jibu: Hapana, haina hukumu moja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kilicho chini ya vifundo vya miguu kiko Motoni.”

Hii ndio Isbaal.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25212/هل-تحريم-الاسبال-مقيد-بالخيلاء-وهل-يشمل-الاكمام
  • Imechapishwa: 17/02/2025