Swali 04: Inajuzu kwenda kwa kuhani, mpiga ramli na wachawi na kuwauliza na kujitibisha kwao kwa kutumia zaituni na mfano wake?
Jibu: Haijuzu kwenda kwa wapiga ramli, wachawi, wanajimu, makuhani na mfano wao. Wala haijuzu kuwauliza wala kuwasadikisha. Wala haijuzu kujitibisha kwao kwa kutumia zaituni wala kitu kingine. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuwaendea, kuwauliza na kuwasadikisha. Kwa sababu wanadai kujua mambo yaliyofichikana, wanawadanganya watu na wanaita katika sababu zinazopelekea kupotea kutokamana na ´Aqiydah. Imesihi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:
“Yeyote atakayemwendea mpiga ramli na akamuuliza juu ya kitu, basi hazitokubaliwa swalah zake nyusiku arobaini.”
Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.
Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Yeyote atakayemwendea mpiga ramli au kuhani akamsadikisha kwa aliyoyasema, basi hakika ameyakufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”
Pia amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hatokamani na sisi yule mwenye kufanya uchawi au akaomba kufanyiwa uchawi, akafanya mkosi au akaomba kufanyiwa mkosi, akafanya ukuhani au akaomba kufanyiwa ukuhani.”
Zipo Hadiyth nyingi zilizokuja kwa maana kama hii.
Yale aliyohalalisha Allaah katika kujitibisha kwa kufanya matabano yanayokubalika Kishari´ah na madawa yaliyo halali kwa wale watu wanaotambulika kuwa na ´Aqiydah na historia nzuri ni yenye kutosheleza na himdi zote njema anastahiki Allaah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Akhtwaau fiyl-´Aqiydah, uk. 11-12
- Imechapishwa: 07/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Kama mtu amelazimika kwenda kwa wachawi na wapiga ramli
Swali: Ni ipi hukumu ya kwenda kwa wachawi na makuhani kwa lengo la matibabu mtu akiwa amelazimika kufanya hivo? Jibu: Haijuzu kwenda kwa makuhani, wachawi na waganga wala kuwauliza. Bali ni lazima kuwazindua, kuwachukulia hatua na kuwakataza. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Yeyote atakayemwendea mpiga ramli au kuhani…
In "Kufuru na aina zake"
09. Kuwaendea makuhani, waganga na wachawi
Kuna mambo yanayofanywa na watu ambayo yanaitia kasoro ´Aqiydah. Kwa mfano kuwaendea wachawi na makuhani kwa ajili ya kutibiwa kwao na kutafuta dawa kwao. Mtu kasibiwa na maradhi na anataka kutibu haya maradhi. Hakuna ubaya kujitibisha. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Enyi waja wa Allaah! Jitibisheni na wala msijitibishe…
In "al-´Aqiydah as-Swahiyhah"
Kwenda kwa mchawi kuhakikisha kama amerogwa
Swali: Je, inafaa kwa mtu kwenda kwa mchawi kujua kama amerogwa au hakurogwa? Jibu: Haijuzu. Ni haramu kuwasadikisha wachawi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Yeyote atakayemwendea mpiga ramli au kuhani akamsadikisha kwa aliyoyasema, basi hakika ameyakufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).” Wachawi hawasadikishwi, hawaendewi wala kuwaheshimishwi. Ni…
In "Uchawi na ukuhani"