Inafaa wanafunzi kusimama pindi mwalimu anapoingia klasini?

Swali: Imepokelewa kuwa siku moja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alilitokea kundi la Maswahabah ambapo wakawa wamesimama kwa ajili yake. Akawaambia:

”Msisimame kama wanavyosimama waajemi wakiadhimishana wao kwa wao.”

a) Ni ipi hukumu ya Uislamu kwa wanafunzi kusimama kwa ajili ya waalimu wakati wanapoingia klasini. Je, ni kitendo kinachojuzu au hapana?

b) Watu kusimamiana wao kwa wao kwenye vikao wakati wa kusalimiana na kupeana mikono ni jambo limekatazwa?

Jibu: Uongofu bora ni wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), uovu wa mambo ni ya kuzua, karne bora ni ile aliyokuwemo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na karne ya kufuatia kama ilivyothibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Katika hili msimamo wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilikuwa wakati anapowajia hawamsimamii kutokana na vile walivyokuwa wanajua kuwa anachukia hilo. Kwa hivyo haifai kwa mwalimu huyu kuwaamrisha wanafunzi kusimama kwa ajili yake. Vilevile haifai kwa wanafunzi kutekeleza akiwaamrisha kufanya hivo kwa kuwa hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (01/148-149)
  • Imechapishwa: 24/08/2020