Swali: Kuna dhambi kwa mwanamke mfungaji kutumia mafuta?

Jibu: Mwanamke hana dhambi akitumia mafuta usoni mwake au kwenginepo katika vitu vinavyompamba au visivyompamba. Muhimu ni kwamba mafuta, kwa aina zake zote, sawa yatumiwe usoni mwake, mgongoni mwake au sehemu nyingine yoyote, hayamuathiri chochote mfungaji na wala hayamfunguzi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/228)
  • Imechapishwa: 12/06/2017