Inafaa kwa mawakala wa Udhhiyah kukata nywele na kucha zao?

Kuhusu ambaye amewakilishwa kumchinjia Udhhiyah mwengine au Waqf ambao ndani yake kuna vichinjwa vya Udhhiyah, hahitaji kuacha nywele, kucha wala ngozi yake. Sio yeye mwenye kuchinja. Hakika mambo yalivyo hilo linamuhusu mchinjaji ambaye amemuwakilisha kazi hiyo. Vivyo hivyo yule aliyetoa Waqf ndiye mwenye kuchinja. Msimamizi wa Waqf ni mwakilishwi na mtekelezaji na sio mchinjaji.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/16859/https://binbaz.org.sa/fatwas/16859/
  • Imechapishwa: 06/06/2024