6- Kumtumia thawabu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tunasema – na Allaah ndiye anajua zaidi – kumtumia thawabu za kisomo cha Qur-aan au thawabu za matendo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni jambo ambalo wanachuoni wametofautiana kwalo. Kuna katika wanachuoni wa Fiqh waliokuja nyuma ambao wamependekeza hilo na wengine wakaonelea kuwa ni Bid´ah. Na hii ndio kauli ya sawa kutokana na sababu mbili:

1- Maswahabah hawakuwa wakifanya hivi.

2- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapata ujira wa kila mwenye kutenda jambo la kheri katika Ummah wake pasi na yule mtendaji kupungukiwa na kitu katika ujira wake. Kwa sababu yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye ambaye ameuongoza Ummah wake katika kila kheri, akawaelekeza na kuwaita kwayo. Mwenye kulingania katika uongofu ana ujira wa mfano wa yule atakayemfuata. Uongofu au elimu aina yoyote ile imepatikana kupitia mikononi mwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo ana ujira mfano wa yule atakayemfuata, sawa ikiwa mtu huyo atamzawadia au asimzawadie. Huu ndio usawa: ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hazawadiwi/kutumiwa kitu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ana mfano wa ujira ulio na Ummah. Kwa hiyo hakuna haja ya kumpa zawadi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (02/726-727)
  • Imechapishwa: 19/05/2020