Swali: Je, inajuzu kumlaani shaytwaan?
Jibu: Ndio, inajuzu kama vile Allaah alivyomlaani. Lakini kujikinga kwa Allaah dhidi ya shari yake ndio bora zaidi. Kwa sababu katika kulaani anaweza kujivuna na kujiona, kama ilivyokuja katika Hadiyth. Lakini mtu anapojikinga kwa Allaah dhidi ya shari yake, shaytwaan hudhoofika na kujinyenyekeza.
Swali: Hiyo Hadiyth ni Swahiyh?
Jibu: Haina tatizo:
“Usiseme ´ameangamia shaytwaan`, bali sema ´kwa jina la Allaah.`”
Maana ni kwamba kujikinga kwa Allaah dhidi ya shari yake ni bora kuliko kumlaani, ingawa Allaah amemlaani na kumfukuza.
Mwanafunzi: Vipi kuhusu Hadiyth inayosema:
“Msimlaani shaytwaan, bali jikingeni dhidi yake.”?
Ibn Baaz: Siijui.
Mwanafunzi: Kuhusu kisa cha Aadam (´alayhis-Salaam) na shaytwaan:
فَلَمَّا آتَاهُمَا صَالِحًا جَعَلَا لَهُ شُرَكَاءَ
“Basi anapowapa mwana mwema asiyekuwa na kasoro, wanamjaalia washirika… ”
Je, kisa hicho ni sahihi?
Ibn Baaz: Maandiko ya Qur-aan yanajulisha kuwa ni kisa cha Aadam na mkewe, kwani Allaah amesema:
هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَجَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا لِيَسْكُنَ إِلَيْهَا ۖ فَلَمَّا تَغَشَّاهَا حَمَلَتْ حَمْلًا خَفِيفًا فَمَرَّتْ بِهِ ۖ فَلَمَّا أَثْقَلَت دَّعَوَا اللَّـهَ رَبَّهُمَا لَئِنْ آتَيْتَنَا صَالِحًا لَّنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ فَلَمَّا آتَاهُمَا صَالِحًا جَعَلَا لَهُ شُرَكَاءَ فِيمَا آتَاهُمَا
“Yeye ndiye aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja na akafanya kutokana nayo mke wake ili apate utulivu. Basi anapomwingilia hubeba mimba khafifu anayotembea nayo. Kisha inapokuwa nzito humwomba Allaah Mola wao ´ukitupa mwana mwema asiyekuwa na kasoro, bila shaka tutakuwa katika wanaoshukuru`. Basi anapowapa mwana mwema asiyekuwa na kasoro, wanamjaalia washirika katika kile Alichowapa.”[1]
Kwa hiyo ni kisa ni cha Aadam na mkewe. Wengine katika Salaf wamesema kinahusu kizazi chake, lakini maandiko ya Qur-aan yako wazi kuwa ni cha Aadam na mkewe.
[1] 7:189-190
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31127/ما-حكم-لعن-الشيطان-وهل-التعوذ-افضل
- Imechapishwa: 05/10/2025
Swali: Je, inajuzu kumlaani shaytwaan?
Jibu: Ndio, inajuzu kama vile Allaah alivyomlaani. Lakini kujikinga kwa Allaah dhidi ya shari yake ndio bora zaidi. Kwa sababu katika kulaani anaweza kujivuna na kujiona, kama ilivyokuja katika Hadiyth. Lakini mtu anapojikinga kwa Allaah dhidi ya shari yake, shaytwaan hudhoofika na kujinyenyekeza.
Swali: Hiyo Hadiyth ni Swahiyh?
Jibu: Haina tatizo:
“Usiseme ´ameangamia shaytwaan`, bali sema ´kwa jina la Allaah.`”
Maana ni kwamba kujikinga kwa Allaah dhidi ya shari yake ni bora kuliko kumlaani, ingawa Allaah amemlaani na kumfukuza.
Mwanafunzi: Vipi kuhusu Hadiyth inayosema:
“Msimlaani shaytwaan, bali jikingeni dhidi yake.”?
Ibn Baaz: Siijui.
Mwanafunzi: Kuhusu kisa cha Aadam (´alayhis-Salaam) na shaytwaan:
فَلَمَّا آتَاهُمَا صَالِحًا جَعَلَا لَهُ شُرَكَاءَ
“Basi anapowapa mwana mwema asiyekuwa na kasoro, wanamjaalia washirika… ”
Je, kisa hicho ni sahihi?
Ibn Baaz: Maandiko ya Qur-aan yanajulisha kuwa ni kisa cha Aadam na mkewe, kwani Allaah amesema:
هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَجَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا لِيَسْكُنَ إِلَيْهَا ۖ فَلَمَّا تَغَشَّاهَا حَمَلَتْ حَمْلًا خَفِيفًا فَمَرَّتْ بِهِ ۖ فَلَمَّا أَثْقَلَت دَّعَوَا اللَّـهَ رَبَّهُمَا لَئِنْ آتَيْتَنَا صَالِحًا لَّنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ فَلَمَّا آتَاهُمَا صَالِحًا جَعَلَا لَهُ شُرَكَاءَ فِيمَا آتَاهُمَا
“Yeye ndiye aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja na akafanya kutokana nayo mke wake ili apate utulivu. Basi anapomwingilia hubeba mimba khafifu anayotembea nayo. Kisha inapokuwa nzito humwomba Allaah Mola wao ´ukitupa mwana mwema asiyekuwa na kasoro, bila shaka tutakuwa katika wanaoshukuru`. Basi anapowapa mwana mwema asiyekuwa na kasoro, wanamjaalia washirika katika kile Alichowapa.”[1]
Kwa hiyo ni kisa ni cha Aadam na mkewe. Wengine katika Salaf wamesema kinahusu kizazi chake, lakini maandiko ya Qur-aan yako wazi kuwa ni cha Aadam na mkewe.
[1] 7:189-190
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31127/ما-حكم-لعن-الشيطان-وهل-التعوذ-افضل
Imechapishwa: 05/10/2025
https://firqatunnajia.com/inafaa-kumlaani-japo-kujilinda-dhidi-yake-ndio-bora-zaidi/