25 – Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba alimwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Nifunze du´aa nitayoomba ndani ya swalah yangu.” Akamwambia: “Sema:
اللّهُـمَّ إِنِّـي ظَلَـمْتُ نَفْسـي ظُلْمـاً كَثـيراً وَلا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْت، فَاغْـفِر لي مَغْـفِرَةً مِنْ عِنْـدِك وَارْحَمْـني إِنَّكَ أَنْتَ الغَـفورُ الرَّحـيم
”Ee Allaah! Hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu dhuluma nyingi na hakuna asamehaye dhambi isipokuwa Wewe. Hivyo basi, nisamehe msamaha kutoka Kwako na unirehemu. Kwani hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]
Imekuja katika tamko la Muslim:
”Nitayoomba nyumbani kwangu.”
MAELEZO
Du´aa hii mja anatafuta ukaribu kwa Allaah (´Azza wa Jall) kwa kutambua mapungufu, madhambi yake, ufukara na kumuhitaji kwake Mola Wake. Ametafuta ukaribu kwa Allaah (´Azza wa Jall) kwa majina mawili miongoni mwa majina Yake; nayo ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.
Ni du´aa tukufu na fadhilah zake ni kubwa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimfunza nayo Abu Bakr as-Swiddiyq, ambaye ndiye mbora wa ummah. Ikiwa Abu Bakr as-Swiddiyq (Rdhiya Allaahu ´anh), ambaye ndiye mtu bora baada ya Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam), anafunzwa du´aa hii, basi watu wengine wana haki zaidi ya kuomba hivo kwa sababu ni wahitaji zaidi. Kwa hivyo mtu asijikwaze kwa matendo yake na siku zote aituhumu nafsi yake kwa mapungufu na afanye matendo mengi ya kheri.
[1] al-Bukhaariy (6326) na Muslim (2705).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 30-31
- Imechapishwa: 05/10/2025
25 – Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba alimwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Nifunze du´aa nitayoomba ndani ya swalah yangu.” Akamwambia: “Sema:
اللّهُـمَّ إِنِّـي ظَلَـمْتُ نَفْسـي ظُلْمـاً كَثـيراً وَلا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْت، فَاغْـفِر لي مَغْـفِرَةً مِنْ عِنْـدِك وَارْحَمْـني إِنَّكَ أَنْتَ الغَـفورُ الرَّحـيم
”Ee Allaah! Hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu dhuluma nyingi na hakuna asamehaye dhambi isipokuwa Wewe. Hivyo basi, nisamehe msamaha kutoka Kwako na unirehemu. Kwani hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]
Imekuja katika tamko la Muslim:
”Nitayoomba nyumbani kwangu.”
MAELEZO
Du´aa hii mja anatafuta ukaribu kwa Allaah (´Azza wa Jall) kwa kutambua mapungufu, madhambi yake, ufukara na kumuhitaji kwake Mola Wake. Ametafuta ukaribu kwa Allaah (´Azza wa Jall) kwa majina mawili miongoni mwa majina Yake; nayo ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.
Ni du´aa tukufu na fadhilah zake ni kubwa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimfunza nayo Abu Bakr as-Swiddiyq, ambaye ndiye mbora wa ummah. Ikiwa Abu Bakr as-Swiddiyq (Rdhiya Allaahu ´anh), ambaye ndiye mtu bora baada ya Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam), anafunzwa du´aa hii, basi watu wengine wana haki zaidi ya kuomba hivo kwa sababu ni wahitaji zaidi. Kwa hivyo mtu asijikwaze kwa matendo yake na siku zote aituhumu nafsi yake kwa mapungufu na afanye matendo mengi ya kheri.
[1] al-Bukhaariy (6326) na Muslim (2705).
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 30-31
Imechapishwa: 05/10/2025
https://firqatunnajia.com/04-ikiwa-abu-bakr-aseme-hivi-sisi-tusemeje/