Swali: Inafaa kumsomea matabano ya Qur-aan mtu kafiri ambaye ni mgonjwa?

Jibu: Ndio. Kisa cha yule raisi wa kabila ambaye alikuwa mgonjwa wakawaomba Maswahabah wamsomee. Wakamsomea kwa sharti wawape jopo la kondoo. Wakamsomea na wakachukua kondoo na Allaah akamponya mgonjwa huyu. Lakini hawakuwatumia kondoo wale mpaka kwanza walipomuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawakubalia jambo hilo na yeye akaomba fungu lake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (107) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatoulahfan-22-06-1441.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020