Swali: Inafaa kumsomea matabano ya Qur-aan mtu kafiri ambaye ni mgonjwa?
Jibu: Ndio. Kisa cha yule raisi wa kabila ambaye alikuwa mgonjwa wakawaomba Maswahabah wamsomee. Wakamsomea kwa sharti wawape jopo la kondoo. Wakamsomea na wakachukua kondoo na Allaah akamponya mgonjwa huyu. Lakini hawakuwatumia kondoo wale mpaka kwanza walipomuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawakubalia jambo hilo na yeye akaomba fungu lake.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (107) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatoulahfan-22-06-1441.mp3
- Imechapishwa: 21/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Kuchukua malipo juu ya kuwafanyia watu matabano
Swali: Tunasikia namna ambavo baadhi ya wenye kutibu kwa Qur-aan ambao wanasoma Qur-aan na du´aa zilizowekwa katika Shari´ah juu ya maji au mafuta masafi kwa ajili ya kutibu uchawi, kijicho na mguso wa ki-shaytwaan. Wanachukua malipo juu ya kazi hiyo. Je, kufanya hivo kunafaa kwa mujibu wa dini? Kusomea juu…
In "Ruqyah - Matabano"
Inafaa lakini haikupendekezwa
Swali: Je, inafaa kwa mgonjwa kumkusudia aliyehifadhi Qur-aan tukufu ili amfanyie matabano? Jibu: Inafaa na wala haipendekezwi kwa sababu ya Hadiyth ya wale watu 70.000[1]. [1] Huswayn bin ´Abdir-Rahmaan amesimulia: “Nilikuwa kwa Sa´iyd bin Jubayr na akasema: “Ni nani kati yenu aliyeona nyota iliyorushwa jana?” Nikasema: “Mimi niliiona”, kisha nikasema kwamba haikuwa…
In "Ruqyah - Matabano"
Kigezo cha matabano yanayofaa
Swali: Je, inajuzu kwa muislamu kutumia aina yoyote ile ya Ruqyah? Jibu: Ruqyah inayojuzu ni ile isiyokuwa na shirki; kama Suurah na Aayah za Qur-aan na Adhkaar zilizothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haijuzu kutumia yale yaliyo na shirki; kama kumkinga mgonjwa kwa majina ya majini na…
In "Ruqyah - Matabano"