Inafaa kukata swalah kwa aliyeswali pembeni na anayenuka harufu mbaya?

Swali: Je, mtu akate swalah yake akiswali karibu na mtu aliyekula kitunguu saumu na akakereka?

Jibu: Amnasihi, amnasihi na kumwambia aondoke na asiswali na watu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha usiswali na watu na kwamba aondoke nyumbani kwake na asiswali na watu na asile kitunguu saumu.

Swali: Lakini akate swalah yake na kwenda mahali pengine ikiwa ameshafunga swalah na anakereka na harufu hii na jambo hilo likamwathiri katika unyenyekevu wake?

Jibu: Ni jambo linahitaji kuangaliwa vyema. Akiweza kutoikata basi asiikate, kwa sababu imeshamuwajibiki kwa kule kuingia ndani yake. Katika hali hiyo inawamujibikia kuikamilisha. Kwa hivyo akiweza kujidhibiti aikamilishe.

Swali: Asipoweza na akaenda maeneo mengine?

Jibu: Ikiwezekana kwake kabla ya kukimiwa swalah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23792/ما-العمل-مع-من-وجد-به-راىحة-الثوم-بالمسجد
  • Imechapishwa: 05/05/2024