Swali: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa mwanamke kuswali Tarawiyh? Je, ailipe anapopata hedhi?

Jibu: Ndio imewekwa katika Shari´ah kwa mwanamke kuswali swalah ya Tarawiyh ima nyumbani kwake au msikitini.

Akipatwa na hedhi asiilipe. Hilo ni kwa sababu mwenye hedhi hatakiwi kulipa si swalah ya faradhi wala ya sunnah. Haikuwekwa katika Shari´ah kuilipa pindi anapopata hedhi. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (14/209)
  • Imechapishwa: 17/06/2017