Swali: Katika baadhi ya shule kunawekwa sehemu ya kuswalia, lakini haiwezekani imamu kusimama mahali pa pekee kiasi kwamba wanaoswali wawe nyuma yake. Hivyo imamu huswali kwenye kona ya chumba, kwa mfano katika safu ya mbele upande wa kushoto, kiasi kwamba upande wake wa kushoto kuna ukuta na upande wake wa kulia kuna safu ya wanaoswali. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Hakuna tatizo. Wakiswali upande wake wa kulia au upande wake wa kulia na kushoto, hakuna tatizo. Ikipatikana nafasi ya imamu kusimama peke yake mbele, hilo ndilo bora zaidi. Lakini kama mahali ni finyu, basi wanaswali upande wake wa kulia na kushoto na nyuma yake, lakini wasimtangulie mbele imamu.
Swali: Lakini imamu anaswali huku upande wake wa kushoto kuna ukuta na safu ipo upande wake wa kulia?
Jibu: Hakuna tatizo, wala hakuna haramu katika hilo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1764/حكم-صلاة-المامومين-عن-يمين-الامام
- Imechapishwa: 27/12/2025
Swali: Katika baadhi ya shule kunawekwa sehemu ya kuswalia, lakini haiwezekani imamu kusimama mahali pa pekee kiasi kwamba wanaoswali wawe nyuma yake. Hivyo imamu huswali kwenye kona ya chumba, kwa mfano katika safu ya mbele upande wa kushoto, kiasi kwamba upande wake wa kushoto kuna ukuta na upande wake wa kulia kuna safu ya wanaoswali. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Hakuna tatizo. Wakiswali upande wake wa kulia au upande wake wa kulia na kushoto, hakuna tatizo. Ikipatikana nafasi ya imamu kusimama peke yake mbele, hilo ndilo bora zaidi. Lakini kama mahali ni finyu, basi wanaswali upande wake wa kulia na kushoto na nyuma yake, lakini wasimtangulie mbele imamu.
Swali: Lakini imamu anaswali huku upande wake wa kushoto kuna ukuta na safu ipo upande wake wa kulia?
Jibu: Hakuna tatizo, wala hakuna haramu katika hilo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1764/حكم-صلاة-المامومين-عن-يمين-الامام
Imechapishwa: 27/12/2025
https://firqatunnajia.com/imamu-kusimama-safu-moja-na-maamuma/