Swali: Je, imamu anaweza kuchelewesha ´ishaa kwa saa moja au zaidi?

Jibu: Hapana. Ikiwa kuchelewesha kunawatia uzito asifanye hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa pindi anapowaona Maswahabah wamekuja msikitini mapema, anaswali mapema, na pindi anapowaona wamekuja wamechelewa, anaswali amechelewa. Anatakiwa kuwazingatia wale maamuma. Lakini akiwa anaswali peke yake au pamoja na mkusanyiko unaopendelea kuchelewesha mpaka katika ile theluthi ya kwanza ya usiku kwa sababu ya kupata thawabu, ni sawa. Ama kuwatia watu uzito kwa sababu ya fadhila si sawa. Katika hali hii awaswalishe pale tu wakati utapoingia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (8) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340429.mp3
  • Imechapishwa: 18/01/2017