Swali: Imamu wa msikiti huchelewa katika swalah ya Fajr na Dhuhr na wakati mwingine hutokea akachelewesha swalah kwa karibu saa moja. Ni kipi unachomnasihi?

Jibu: Haifai kwa imamu kuchelewesha swalah, si swalah ya Dhuhr, Fajr wala swalah nyingine yoyote. Kwa sababu ni jukumu lake kutofanya hivo. Wala haitakiwi kuchelewesha kukimu isipokuwa kuhusu swalah ya ´Ishaa. Kwani hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwaona  wamekwishahudhuria, basi anaswali kwa kuharakisha, na akiwaona wamechelewa, basi anaichelewesha[1]. Kuhusu swalah nyenginezo, bora ni kuswali mapema. Hata hivyo imamu anatakiwa kuzingatia zile swalah ambazo zinakuwa na Raatibah kabla yake ili awape watu muda wa kutosha wa kutawadha na kuziswali swalah hizi zinazopendeza.

[1] al-Bukhaariy.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/191)
  • Imechapishwa: 21/05/2026