Anayempa rambirambi ndugu yake aliyefikwa na msiba

Hapana shaka yoyote kwamba ni jambo limesuniwa pole jamaa na wengineo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakuna muumini yeyote anayempa pole ndugu yake kutokana na msiba uliyompata isipokuwa Allaah (´Azza wa Jall) humvisha vazi la heshima siku ya Qiyaamah.”[1]

Lengo la rambamba ni kumtia nguvu yule aliyepatwa na msiba na kumkumbusha kufanya subira. Miongoni mwa rambirambi za kumpa aliyepatwa na msiba ni kumwambia:

اصبر و احتسب، فإن لله ما أخذ، و له ما أبقى، و كل شيء عنده بأجل مسمى

“Subirini na tarajieni malipo kutoka kwa Allaah. Ni Chake Allaah alichokitwaa na Yeye Chake alichokibakiza na kila kitu Kwake kina muda maalum.”

Akiona kuwa ana mahuzuniko makubwa basi hapana vibaya akaongeza zaidi ya hapo.

[1] Ibn Maajah (1601). Nzuir kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (1311).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/362)
  • Imechapishwa: 21/05/2026