Swali: Ni ipi hukumu ya adhaana kwa wasafiri?
Jibu: Wanazuoni wametofautiana juu ya jambo hili. Maoni ya sawa ni kwamba ni wajibu kwa safiri kuadhini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Maalik bin al-Huwayrith (Radhiya Allaahu ´anh) pindi walipokuwa wanasafiri kutokea nyumbani kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Utapofika wakati wa swalah, basi aadhini mmoja wenu na mkubwa wenu aswalishe.”[1]
Jengine ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kamwe hakuach kuadhini wala kukimu, ni mamoja katika hali ya safari wala ya wenyeji. Alikuwa akimwamrisha Bilaal (Radhiya Allaahu ´anh) aadhini wakati wa safari yake.
[1] al-Bukhaariy (628).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/160)
- Imechapishwa: 22/05/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya adhaana kwa wasafiri?
Jibu: Wanazuoni wametofautiana juu ya jambo hili. Maoni ya sawa ni kwamba ni wajibu kwa safiri kuadhini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Maalik bin al-Huwayrith (Radhiya Allaahu ´anh) pindi walipokuwa wanasafiri kutokea nyumbani kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Utapofika wakati wa swalah, basi aadhini mmoja wenu na mkubwa wenu aswalishe.”[1]
Jengine ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kamwe hakuach kuadhini wala kukimu, ni mamoja katika hali ya safari wala ya wenyeji. Alikuwa akimwamrisha Bilaal (Radhiya Allaahu ´anh) aadhini wakati wa safari yake.
[1] al-Bukhaariy (628).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/160)
Imechapishwa: 22/05/2026
https://firqatunnajia.com/ni-ipi-hukumu-ya-adhaana-kwa-wasafiri/