Imamu anasoma nje ya swalah ili kujazia aweze kukhitimu Qur-aan

Swali: Baadhi ya maimamu hawakusahilikiwa kukhitimu Qur-aan katika kisimamo cha Ramadhaan. Baadhi yao wakaendelea kusoma nje ya swalah ili aweze kukhitimu Qur-aan mpaka itapofika tarehe 29. Je, hilo lina msingi wowote katika Shari´ah safi?

Jibu: Sijui msingi wowote juu ya hilo. Sunnah ni imamu aweze kuwasikilizisha waswaliji katika kisimamo cha Ramadhaan Qur-aan yote ikisahilika kufanya hivo pasi na kuwatia uzito. Ikiwa haikusahilika kufanya hivo hakuna neno hata kama hawakukhitimu. Imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo amesema:

“Atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”[1]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

[1] Muslim (1718).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/34)
  • Imechapishwa: 23/05/2018