Swali: Je, waswaliji wanatakiwa kumzindua imamu pindi anaposoma kwa sauti katika swalah za kusoma kimyakimya au kinyume chake?
Jibu: Ndio. Akiendelea kusoma namna hiyo, wanatakiwa kumzindua.
Swali: Je, analazimika kuleta sujuud ya kusahau kwa ajili ya jambo hilo?
Jibu: Inapendeza. Halazimiki kufanya hivo, lakini inapendeza.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
- Imechapishwa: 21/05/2023