Imamu anamaliza kuswali kabla ya kumaliza Tashahhud

Swali: Baadhi ya watu wa kawaida wanapomaliza kuleta Tashahhud na imamu bado amekaa wanairudia kwa mara nyingine. Walipoambiwa kuacha hivo, akasema kuwa yeye anapenda kuirudia mara ya pili na mara ya tatu.

Jibu: Hapana. Amswalie Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya Tashahhud ya kwanza. Iwapo atairudia haina neno.

Swali: Ikiwa imamu anafanya haraka katika Tashahhud na asimuwahi?

Jibu: Akamilishe Tashahhud.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23782/ما-يفعل-الماموم-لو-اطال-الامام-التشهد
  • Imechapishwa: 26/04/2024