Imamu ana kigugumizi kinachoiharibu al-Faatihah

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali nyuma ya imamu ambaye ana kigugumizi? Matokeo yake ni kwamba anabadili baadhi ya herufi za Qur-aan na maneno yanatoka yakiwa si sahihi. Kwa mfano “as-Swiraatw” anasema “as-Swiraat” na “al-Mustaqiym” anasema “al-Muthtaqiym”?

Jibu: Naona kuwa imamu huyu si halali kwake kuwaongoza watu. Kwa sababu mabadilisho haya yanabadilisha maana. Ang´olewe kuwa imamu na badala yake awekwe mtu mwingine aliyesamilika.

Lakini tukikadiria kuwa mtu amejiunga naye ilihali hajui kisha akakamilisha swalah, na huyu aliyejiunga naye anasoma al-Faatihah kivyake kisomo ambacho ni cha sawa, hawajibiki kuirudi swalah yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/951
  • Imechapishwa: 12/12/2018