Swali: Mwezi wa Dhul-Hijjah una fadhila zepi ?

Jibu: Mwezi wa Dhul-Hijjah dhahiri ni kwamba makusudio ni yale masiku kumi. Mtu anapaswa katika masiku haya kumi akithirishe matendo mema. Kama vile swalah, swadaqah na swawm pia. Afunge yale masiku tisa. Vilevile akithirishe matendo mengine yote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna masiku ambayo matendo mema yanapendwa zaidi na Allaah ndani yake kama  masiku haya kumi.” Wakasema: “Hata Jihaad katika njia ya Allaah?” Akajibu: “Hata Jihaad katika njia ya Allaah. Isipokuwa mtu ambaye ametoka na nafsi yake na mali yake na asirudi na chochote katika hayo.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/949