Imamu amesoma kwa sauti katika swalah za kusoma kimyakimya

Swali: Je, imamu alete Sujuud-us-Sahuw ikiwa atasoma kwa sauti katika swalah ya Dhuhr kisha baadaye akakumbuka na akasoma kimyakimya?

Jibu: Ndio, katika hali hii kuleta Sujuud-us-Sahuw itakuwa Sunnah. Ikiwa hakuileta swalah ni sahihi.

Swali: Je, ni lazima kwa imamu kuleta Sujuud-us-Sahuw akisahau kuleta Takbiyr kwa sauti wakati wa kwenda kwenye Rukuu´ na Sujuud?

Jibu: Imependekezwa kwake kuileta. Maadamu amesema “Allaahu Akbar” hata kama ni kwa siri amefanya ambalo ni wajibu. Lakini hata hivyo asujudu kwa kutokuisema kwa sauti.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (58) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-01-14.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020