Imamu amesahau kusujudu Sujuud ya pili katika Rak´ah ya mwisho

Swali: Imamu wetu amesahau kuleta Sujuud katika Rak´ah ya nne. Baada ya Tasliym mkusanyiko ukamkumbusha ambapo akasujudu moja kwa moja na wala hakukaa kati ya Sujuud mbili. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ameshakaa tayari. Wanamwambia wakati ameshakaa chini. Anatakiwa kuleta Sujuud ya pili, kisha Tasliym na halafu Sujuud ya kusahau.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tahid-25-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017