Sa´iyd bin Mansuur bin Shu´bah, Haafidhw, Imaam, Shaykh wa msikiti Mtakatifu, Abu ´Uthmaan al-Khuraasaaniy al-Marwaziy na inasemekana at-Twalaqaaniy, kisha al-Balkhiy, kisha al-Makkiy. Mtunzi wa ”as-Sunan”.

Baadhi ya aliowasikia Khuraasaan, Hijaaz, ´Iraaq, Misri, Shaam na Kurdistan ni pamoja na Maalik bin Anas, al-Layth bin Sa´d, Hushaym, Ismaa´iyl bin ´Ayyaash, al-Fudhwayl bin ´Iyaadhw, Sufyaan bin ´Uyaynah na wengineo.

Alikuwa mkweli, mwaminifu na chombo cha elimu.

Miongoni mwa waliopokea kutoka kwake ni pamoja na Ahmad bin Hanbal, Abu Thawr al-Kalbiy, Abu Muhammad ad-Daarimiy, Abu Bakr al-Athram, Abu Daawuud, Muslim, Muhammad bin Yahyaa adh-Dhuhaliy, Abu Haatim ar-Raaziy na wengineo.

Salamah bin Shabiyb amesema:

”Nilimtaja Sa´iyd bin Mansuur mbele ya Ahmad bin Hanbal ambapo akamsifu na akamuadhimisha.”

Abu Haatim ar-Raaziy amesema:

“Ni mwaminifu na ni miongoni mwa watu mairi imara waliokusanya na wakatunga.”

Harb al-Kirmaaniy amesema:

“Sa´iyd bin Mansuur alitusomea karibu Hadiyth 100.000 kutoka kichwani mwake.”

Nasema: Alikuwa takriban na miaka 80 wakati alipofariki Makkah Ramadhaan mwaka 227.

Harb bin Ismaa´iyl amesema:

”Ametunga vitabu na akavifanya kwa kiwango kikubwa.”

Ya´quub al-Fasaawiy amesema:

“Alikuwa anapoona kwenye kitabu chake kosa, basi hajirejei.”

Nasema: Linganisha haya na rafiki yake Imaam Yahyaa bin Yahyaa al-Khuraasaaniy ambaye alikuwa akiiacha Hadiyth nzima pindi anapotilia mashaka herufi yake.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (10/586-595)
  • Imechapishwa: 29/09/2020