Muhammad bin Yahyaa bin ´Abdillaah bin Khaalid bin Faaris bin Dhu-ayb. Imaam, Allaamah, Haafidhw, Shaykh-ul-Islaam na mwanachuoni wa mashariki na imamu wa Ahl-ul-Hadiyth Khuraasaan. Abu ´Abdillaah adh-Dhuhliy an-Niysaabuuriy.
Alizaliwa mwaka wa 170.
Baadhi ya waliosikia kutoka kwake ni pamoja na Hafsw bin ´Abdillaah, Hafsw bin ´Abdir-Rahmaan, al-Husayn bin al-Waliyd, Makkiy bin Ibraahiym na wengineo.
Miongoni mwa wale alioandika kutoka kwao huko Aswbahaan ni pamoja na ´Abdur-Rahmaan bin Mahdiy. Haya yamesemwa na al-Haakim.
Alikusanya elimu ya az-Zuhriy na ndio maana aliitwa ”az-Zuhriy” na pia ”adh-Dhuhliy”. Elimu na utukufu ulikomekea kwake. Alikuwa na utukufu wa ajabu huko Niysaabuur kama utukufu aliokuwa nao Imaam Ahmad Baghdaad na Maalik huko al-Madiynah.
Kuna wengi waliopokea kutoka kwake baadhi yao ikiwa ni Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy, Sa´iyd bin Mansuur, Abu Zur´ah, Abu Haatim, Abu ´Iysaa at-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Imamu wa maimamu Ibn Khuzaymah, Makkiy bin ´Abdaan, Abu ´Awaanah, Abu Bakr bin Ziyaad an-Niysaabuuriy na Muslim, ambaye alipokea kiwango kikubwa kutoka kwake.
Ibn Abiy Haatim amesema:
”Baba yangu aliandika kutoka kwake huko ar-Rayy na akasema: ”Ni mwaminifu.”
Halafu Ibn Abiy Haatim akasema:
”Ni mmoja katika maimamu wa waislamu.”
al-Khatwiyb amesema:
”Alikuwa ni mmoja katika maimamu watambuzi na mabingwa wa kuhifadhi. Aliziandika Hadiyth za az-Zuhriy na akafanya vyema. Ahmad bin Hanbal alikuwa akimsifu na akieneza fadhilah zake.”
Abu ´Amr na Ahmad bin Naswr al-Khaffaaf amesema:
”Nilimuona ndotoni Muhammad bin Yahyaa baada ya kufa kwake. Nikamwambia: ”Allaah amekufanya nini?” Akasema: ”Amenisamehe.” Nikasema: ”Amezifanya nini Hadiyth zako?” Akasema: ”Zimeandikwa kwa maji ya dhahabu na zikanyanyuliwa ´Illiyyuun[1].”
Abu ´Amr al-Mustamiliy amesema:
”Nilimwendea Ahmad bin Hanbal. Akanambia: ”Unatokea wapi?”Nikasema: “Niysaabuur.”Akasema: “Je, Abu ´Abdilalah Muhammad bin Yahyaa ana vikao?” Nikasema: “Ndio.” Akasema: “Laiti angelikuwa kwetu, basi tungemfanya kuwa imamu katika Hadiyth.”
Sa´iyd bin Mansuur amesema:
”Nilisema kumwambia Yahyaa bin Ma´iyn: ”Kwa nini unakusanya Hadiyth za az-Zuhriy?” Ndipo akasema: “Muhammad bin Yahyaa ametutosheleza kufanya hivo.”
an-Nasaa´iy amesema:
“Ni mwaminifu na mwenye kuaminiwa.”
Ibn Abiy Daawuud amesema:
“Muhammad bin Yahyaa ametuhadithia na alikuwa ni kiongozi katika Hadiyth.”
Abu ´Amr al-Mustamiliy amesema:
“Nimemsikia Muhammad bin Yahyaa akisema: “Nimemfanya Ahmad bin Hanbal kuwa imamu katika yale yaliyoko kati yangu mimi na Mola wangu.”
Muhammad bin Yahyaa amesema:
“Watu ambao ni imara zaidi niliowaona ni wanne; ´Abdur-Rahmaan, Wahb bin Jariyr, Yaziyd bin Haaruun na Sulaymaan bin Harb.”
Muhammad bin Yahyaa amesema:
”´Aliy al-Madiyniy alinambia: ”Wewe ndiye mrithi wa az-Zuhriy.”
Imamu wa maimamu Ibn Khuzaymah amesema:
“Muhammad bin Yahyaa adh-Dhuhliy, imamu wa wakati wake, ametuhadithia, Allaah amkaze Peponi pmaoja na wenye kumpenda.”
Ibn-ush-Sharqiy amesema:
“Hakuna yeyote aliyetoka Khuraasaan kama mfano Muhammad bin Yahyaa. Alifariki mwaka wa 258.”
Abu ´Amr al-Mustamiliy amesema:
“Aliishi miaka 86.”
[1] Imaam ´Abdur-Rahmaan as-Sa´diy (Rahimahu Allaah) amesema:
”´Illiyyuun ni sakafu ya Pepo.” (Tafsiyr as-Sa´diy, uk. 916)
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (12/273-285)
- Imechapishwa: 01/10/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)