Imaam Muhammad bin Ibraahiym kuhusu sherehe ya krismasi na kupeana zawadi

Tumepata khabari ya kwamba kuna wafanyabiashara mwaka jana waliyoingiza karama za krismasi katika uhusiano na mwaka mpya wa kinaswara. Miongoni mwa karama hizi kulikuwa miti ya krismasi ambayo baadhi ya raia waliwapa wageni wa kinaswara katika nchi yetu kama ishara ya ushiriki wa sikukuu yao.

Hichi ni kitendo cha dhambi ambacho watu hawa kamwe wasingejiingiza humo [laiti wangejua hukumu yake]. Sina shaka ya kwamba mnajua kuwa hili ni haramu na kwamba wanachuoni wote wamesema kuwa ni haramu kushiriki kwenye sherehe za makafiri. Natumaini ya kwamba mnatambua kuwa ni haramu kuagiza zawadi na kila kile ambacho ni maalumu kwa sherehe zao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahim Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawa (3/105)
  • Imechapishwa: 05/10/2020