Swali: Kuna imamu Ufaransa anaruhusu kupeana mikono na wanawake wa idara kwa sababu eti anachelea matatizo kama kwa mfano kufungwa kwa msikiti na mengineyo. Kwa ajili hiyo anapeana nao mikono. Je, kitendo chake hichi kinakubalika Kishari´ah?

Jibu: Hapana, hakikubaliki Kishari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwahi kupeana mikono na wanawake hata siku moja. Alikuwa akiwabai wanawake kwa maneno. Anawabai wanaume kwa kupeana nao mikono. Kuhusu wanawake anawabai kwa maneno na wala hapeani nao mikono.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (88) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahssat.mp3
  • Imechapishwa: 10/09/2018