Swali: Ni ipi hukumu ya kupiga kura na kushiriki katika uchaguzi katika nchi isiyokuwa ya Kiislamu kwa ajili ya kufikia manufaa na kuzuia madhara, kuchagua madhara madogo na kufanya sauti ya waislamu iweze kusikika? Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) ameshatupa fatwa inayojuzisha USA, lakini baadhi ya watu wanasema kuwa ni haramu. Unasemaje?

Jibu: Nimeshajibu swali hili miaka mingi ya nyuma, ima Haram au kipindi ”Nuur ´alaad-Darb”.

Muislamu anatakiwa kufanya kazi juu ya manufaa ya waislamu, kitu ambacho hakiwezi kupatikana kwa kwenda kinyume na amri ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kitu ambacho hukumu yake haikutajwa ndani ya Qur-aan na Sunnah lakini ikabainika kuwa kinawanufaisha waislamu, basi kitatakiwa kufanyiwa kazi. Kama mfano wa uchaguzi. Ikiwa yule anayechaguliwa anahakikisha waislamu kunufaika zaidi kuliko wanavofanya wagombea wengine na hivyo wakashiriki katika jambo hilo, basi hakuna vibaya kwao. Wanatakiwa kujitahidi kiasi wanachoweza. Pengine kusipatikane kile wanachokitaka, lakini ikiwa wana matarajio kuwa mtu huyo atawanufaisha waislamu zaidi kuliko wengine, basi hapana neno wala uharamu.

Baadhi ya nchi za magharibi zina idadi kubwa ya waislamu. Ikiwa watasaidiana na wakawa kitu kimoja, basi uchaguzi wao una athari nzuri. Kwa mfano nchi ina waislamu milioni kumi ambapo wakampigia kura mtu mwenye busara, ambaye wanamuona kuwa ni mkweli, mtekelezaji na mwenye kunufaisha ambaye hachukulii dini kutokana na matamanio yake. Hapana neno.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin Swaalih al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.salafi-dawah.com/uploads/1/5/0/0/15007852/shaykh_al-luhaydaan_-_regarding_voting_to_remove_harm_or_bring_benefit.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2022