Ikiwa Muhrim hana uwezo wa kununua shuka ya chini

Swali: Bora kwa mtu avae suruwali au akope na anunue shuka ya chini ikiwa hamiliki pesa katika hijjah?

Jibu: Anunue shuka ya chini. Muhrim ameamrishwa kununua shuka ya chini, isipokuwa akishindwa hapo ndipo atavaa suruwali.

Swali: Hata kama atakopa?

Jibu: Hapana, sio lazima akope:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Ikiwa hana namna isipokuwa kukopa basi avae suruwali. Shuka ya chini ni nzuri na yenye kufunika na vyema zaidi kuliko suruwali, kwa sababu suruwali inaweza kuonyesha umbile la viungo visivyotakiwa kuonekana. Wakati mwingine inakuwa yenye kubana kama ambaye hakuvaa. Hata hivyo shuka ya chini inafunika vyema zaidi. Kwa ajili hiyo miongoni mwa desturi za waarabu wanavaa kikoi zaidi kuliko suruwali.

[1] 64:16

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24092/حكم-السروال-لمن-لا-يملك-ثمن-الازار-بالحج
  • Imechapishwa: 27/08/2024