Swali: Ambaye anaswali na kufunga Ramadhaan peke yake na miezi mingine anaswali ijumaa peke yake?
Jibu: Huyu ni kafiri. Kwa mujibu wa maoni sahihi ya wanazuoni ni kwamba ni kafiri. Ambaye haswali isipokuwa Ramadhaan au siku ya ijumaa peke yake ni kafiri. Hapana shaka kwamba ni kafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule mwenye kuiacha amekufuru.”[1]
Ameipokea Ahmad na watunzi wa Sunan kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
Imekuja katika Hadiyth ya Jaabir kwa Muslim:
“Hakika baina ya mtu na baina ya shirki na kufuru ni kuacha swalah.”[2]
al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu kuwapiga vita viongozi ambao wanaenda kinyume na amri ambapo akajibu:
”Hapana, isipokuwa mkiona kufuru ya wazi ambayo mko na dalili kwayo kutoka kwa Allaah.”[3]
Akasema katika tamko jengine:
”… muda wa kuwa wanatekeleza kati yenu swalah.”
Kwa hivyo ikafahamisha kuwa kuswali kunamkinga mtu. Ameita ”ukafiri wa wazi” kule kuacha swalah na hakumlindi mtu.
[1] at-Tirmidhiy (2621) ambaye amesema:
”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh na geni.”
an-Nasaa´iy (463), Ibn Maajah (1079) na Ahmad (22937).
[2] Muslim (82).
[3] al-Bukhaariy (7055) na Muslim (1709).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24094/حكم-من-يصلي-ويصوم-في-رمضان-فقط
- Imechapishwa: 27/08/2024
Swali: Ambaye anaswali na kufunga Ramadhaan peke yake na miezi mingine anaswali ijumaa peke yake?
Jibu: Huyu ni kafiri. Kwa mujibu wa maoni sahihi ya wanazuoni ni kwamba ni kafiri. Ambaye haswali isipokuwa Ramadhaan au siku ya ijumaa peke yake ni kafiri. Hapana shaka kwamba ni kafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule mwenye kuiacha amekufuru.”[1]
Ameipokea Ahmad na watunzi wa Sunan kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
Imekuja katika Hadiyth ya Jaabir kwa Muslim:
“Hakika baina ya mtu na baina ya shirki na kufuru ni kuacha swalah.”[2]
al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu kuwapiga vita viongozi ambao wanaenda kinyume na amri ambapo akajibu:
”Hapana, isipokuwa mkiona kufuru ya wazi ambayo mko na dalili kwayo kutoka kwa Allaah.”[3]
Akasema katika tamko jengine:
”… muda wa kuwa wanatekeleza kati yenu swalah.”
Kwa hivyo ikafahamisha kuwa kuswali kunamkinga mtu. Ameita ”ukafiri wa wazi” kule kuacha swalah na hakumlindi mtu.
[1] at-Tirmidhiy (2621) ambaye amesema:
”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh na geni.”
an-Nasaa´iy (463), Ibn Maajah (1079) na Ahmad (22937).
[2] Muslim (82).
[3] al-Bukhaariy (7055) na Muslim (1709).
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24094/حكم-من-يصلي-ويصوم-في-رمضان-فقط
Imechapishwa: 27/08/2024
https://firqatunnajia.com/anayeswali-ijumaa-peke-yake/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)