Swali: Ikiwa ni siku ya ijumaa, je, msafiri anakusanya na kufupisha swalah ya Dhuhr na ´Aswr pamoja?

Jibu: Msafiri hana wajibu wa swalah ya ijumaa. Bali ataswali Dhuhr. Aidha hapana vibaya kujumuisha kati ya Dhuhr na ´Aswr. Lakini ikiwa msafiri ataswali ijumaa pamoja na watu katika mji wowote, basi hatakusanya nayo ´Aswr. Bali ataswali ´Aswr ndani ya wakati wake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/215)
  • Imechapishwa: 15/03/2026