Idadi ya chini ya swalah ya mkusanyiko

Swali: Kuna mtu amepitwa na swalah ya mkusanyiko ambapo akarudi nyumbani. Je, amswalishe mke wake swalah ya mkusanyiko?

Jibu: Haizingatiwi ni swalah ya mkusanyiko. Hakuna neno akamswalisha mke wake. Ama kusema kwamba inazingatiwa ni mkusanyiko pamoja na mke wake sivyo hivyo. Idadi ya chini ya swalah ya mkusanyiko ni wanamme wawili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (105) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/20-03-1441-H-%20igah.mp3
  • Imechapishwa: 09/10/2020