Madhambi yetu ni mengi. Tukitawalishiwa watawala wakandamizaji, basi ni kutokana na madhambi yetu:

وَكَذَٰلِكَ نُوَلِّي بَعْضَ الظَّالِمِينَ بَعْضًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ

”Na hivyo ndivyo Tunavyowafanya baadhi ya madhalimu kuwa marafiki wao kwa wao kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.”[1]

Da´wah ya Ahl-us-Sunnah ni yenye kuitakia kheri jamii. Ndugu zetu walioingizwa gerezani Aden wamefanya kosa gani? Watu wote mpaka wakumonusti na wanajamaa wamepata msamaha. Wanatukandamiza sisi Ahl-us-Sunnah, lakini tunasubiri. Tunasubiri. Sunnah ndio inayofungua njia.

[1] 06:129

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=18
  • Imechapishwa: 09/10/2020