Takfiyr za leo hayana lolote kuhusiana na Uislamu

Swali: Naketi na baadhi ya watu ambao wanasema kuwa wanachuoni wakubwa ni makafiri kwa sababu wanawasapoti washirikina na washirika wao na wanawafunza na kuwalea vijana juu ya jambo hilo na khaswa baada ya kutoka fataawaa zinazoharamisha ulipuaji katika miji ya makafiri. Vipi unaraddi utata huu?

Jibu: Mosi ni kwamba Takfiyr sio katika mambo sahali. Kwa ajili hiyo ndio maana Allaah (´Azza wa Jall) anakufurisha kwa njia ya sifa na sio kwa njia ya mtu mmojammoja. Vivyo hivyo hukumu nyenginezo. Mtaona namna ambavyo hukumu za Qur-aan zimekuja kwa njia ya sifa. Ndio maana Allaah (Jalla wa ´Alaa) anasema:

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ

“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.” (al-Maaidah 05:44)

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ

“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu.” (al-Maaidah 05:45)

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ

“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki.” (al-Maaidah 05:47)

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Naapa kwa Mola wako! Hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu katika yale wanayozozana kati yao kisha wasipate katika nyoyo zao uzito katika yale uliyohukumu na wajisalimishe ukweli wa kujisalimisha.” (an-Nisaa´ 04:65)

Takfiyr sio katika mambo mepesi. Kujengea juu ya hayo pindi mtu anasikia mtu maalum anakufurishwa na kwamba hilo linaingia katika misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, basi anatakiwa kutambua kwamba haifai kumkufurisha mtu kwa dhati yake. Hata hivyo hakuna kizuizi kama ni kwa njia ya sifa na kusema kwamba mwenye kufanya jambo fulani basi hukumu yake ni kadhaa. Kuhusu kumkufurisha mtu kwa dhati yake haijuzu. Ama yale yanayoenea hii leo kwenda mbali zaidi katika mambo ya Takfiyr hayana lolote kuhusiana na Uislamu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=143186
  • Imechapishwa: 09/10/2020