Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

وَلَا تَلْبِسُوا الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُوا الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

“Na wala msichanganye haki kwa batili na mkaficha haki ilihali mnajua.”[1]

Amewakataza mambo mawili:

1- Kuchanganya haki kwa batili.

2- Kuficha kubainisha haki.

Kwa sababu malengo kwa watu waliopewa Kitabu na wasomi ni wao kuipambanua haki na kuidhihirisha ili wapate kuongoka kwayo waongofu, wajirudi wapotofu na hoja ipate kusimama dhidi ya wale wakaidi. Kwa sababu Allaah amepambanua Aayah na kuweka wazi hoja Zake kwa ajili ya kupambanua haki kutokamana na batili, ipate kuwa wazi njia ya waongofu kutokamana na njia ya wahalifu.

Yule mwenye kutendea kazi haya miongoni mwa wanachuoni ni katika makhalifa wa Mitume na waongozaji wa Ummah. Na yule mwenye kuichanganya haki kwa batili kwa njia ya kwamba asipambanua hichi kutokamana na hichi na wakati huohuo akawa ni mwenye kulijua hilo, akaificha haki ambayo anaijua na asiamrishe kudhihirishwa, basi huyo ni miongoni mwa walinganizi wa Motoni. Kwa sababu watu hawaongoki katika mambo yanayohusu dini yao pasi na wanachuoni wao. Kwa hiyo zichagulieni nafsi zenu moja katika hali hizo mbili.

[1] 02:42

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, uk. 42
  • Imechapishwa: 30/06/2020