Swali: Ni ipi hukumu ya kucheza visa vya kinabii na vya Qur-aan kwa njia ya viwiliwili kwa filamu za katuni? Huenda wakati mwingine wakazidisha juu yake na wakabadilisha kama kisa cha kijana wa Ukhduud, kisa cha watu wa ndovu ambapo kukachorwa picha ya ndovu au kisha cha mwanachuoni, mfalme na mchawi? Ni ipi hukumu ya kutumia dufu katika mfano wa mambo kama haya?

Jibu: Kwanza visa hivi wakati mwingine huenda vikawa si sahihi. Ni vipi mtu atajengea kwa kisichokuwa sahihi?

Pili ni kwamba mimi nachelea yule mtu mwenye kuwachora na akafanya viwiliwili vyao akaombwa alete dalili kama picha ya kijana na ya mchawi yule ilikuwa inafanana hivo? Leta dalili kama watu wa Ukhduud walikuwa wanafanana hivo? Hawana utambuzi wa hilo.

Uumbaji bado unaendelea kushuka. Mwanaadamu hapo kabla alikuwa mkubwa. Aadam aliumbwa urefu wake ulikuwa unafika mbinguni dhiraa sitini. Imepokelewa katika Hadiyth nyingine kwamba urefu wake ulikuwa dhiraa saba. Bado umbile la viumbe linaendelea kupungua mpaka limekuwa kama tulivyo hivi sasa. Ni kipi kilichowajuza kwamba watu wa Ukhduud walikuwa namna hii?

Kwa ajili hiyo mimi naonelea kuwa uchaji Allaah ni mtu kutofanya mambo hayo. Inatosha kuelezea kwa maneno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/936
  • Imechapishwa: 04/12/2018