Hukumu ya kuswalia kipomoko kabla ya kupuliziwa roho

Swali: Shaykh ambaye yuko katika kitongoji chetu amefutu ya kwamba kipomoko kilichokufa baada ya miezi mitatu kinaoshwa, kinavikwa sanda na kuswaliwa. Je, amepatia kwa yale aliyosema:

Jibu: Hakupatia kwa yale aliyosema. Kwa sababu kipomoko kilichoporomoka kabla ya kupuliziwa roho sio mtu na hakitofufuliwa. Watafufuliwa wale waliopuliziwa roho, jambo ambalo halitimii kabla ya miezi mine.

Kwa ajili hio nataraji muuliza atambainishia yule aliyejibu swali kwamba fatwa hii sio sahihi. Kipomoko kinachoswaliwa ni kile kilichopuliziwa roho. Ama kabla ya hapo hakiswaliwi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/934
  • Imechapishwa: 04/12/2018