Swali: Lau mwanamke ataswali nyuma ya wanaume kisha akakosea imamu, akakosea katika kusoma kwake Qur-aan na asisahihishwe. Lakini mwanamke akawa anajua hilo. Je, anaweza akamsahihisha?
Jibu: Ikiwa hili ni katika al-Faatihah, ni lazima kwake mwanamke kumsahihisha. Kwa kuwa lau imamu atakosea al-Faatihah swalah haitosihi. Ikiwa sio al-Faatihah na wanaume wakawa hawajui na wala hawatoshangazwa akiongea mbele yao, amrekebishe na hakuna neno. Kwa kuwa sauti ya mwanamke sio ´Awrah. Dalili kuonesha kuwa sio ´Awrah ni maneno Yake (Ta´ala):
يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِّنَ النِّسَاءِ ۚ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا
“Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote yule katika wanawake; mkiwa na taqwa, basi msilainishe kauli asije akaingiwa na tamaa yule ambaye moyoni mwake mna maradhi na semeni kauli inayokubalika.” (33:32)
Makatazo ya kutolainisha sauti ni dalili inayoonesha kuwa inajuzu kuongea.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (13 A)
- Imechapishwa: 14/09/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket