Ibn ´Uthaymiyn mfungaji aliyemjamii mke wake akifikiria kuwa inajuzu

Swali: Kuna mtu alikuwa anaamini kuwa kufanya jimaa mchana wa Ramadhaan pasi na kumwaga hakuharibu swawm. Ana nini juu yake?

Jibu: Ikiwa aina ya mtu kama huyu kweli hajui, bi maana si msomi kihakika na hakuwahi kusikia kupata elimu yoyote kwamba tendo hili linaharibu swawm, swawm yake ni sahihi na haikuharibika na kadhalika haimlazimu yeye kulipa kama jinsi haimlazimu kutoa kafara. Ama ikiwa aina ya mtu kama huyu anajua, kwa mfano aliwahi kusoma na akajua au alisikia kwa watu, hana udhuru. Muhimu ni kwamba, ikiwa ni mkweli kwa ujinga wake na aina kama yeye hajui, hana lolote juu yake, si kulipa, kafara wala madhambi. Allaah (Ta´ala) amesema:

رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا

“Mola wetu usituchukulie tukisahau au tukikosea.” (02:286)

Vilevile Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) katika zama za Mtume walikula wakati walipofikiria kuwa jua limeshazama halafu baada ya hapo jua likachomoza, hata hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwaamrisha kulipa kwa kuwa hawakuwa wanajua wakati. Kula na kunywa ni kama jimaa, hakuna tofauti kati yake kwa sababu yote mawili yanaharibu swawm. Ikiwa swawm haiharibiki kwa kula pasi na mtu kujua, kadhalika jimaa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 02
  • Imechapishwa: 23/09/2020