Mtu asifanye siku za swawm zake na za kula ikawa sawasawa. Lakini hata hivyo sisi – na tunamuomba Allaah afya – tunafanya siku za swawm zetu na za kula kwetu sawasawa. Bali baadhi ya watu wanafanya siku za swawm zao kuwa duni kuliko siku za kula kwao. Utaona analala kuanzia Dhuhr mpaka ´Aswr, ´Aswr mpaka Maghrib. Pengine akaacha swalah ya Dhuhr na ´Aswr na kuzikidhi atapoamka wakati wa Maghrib. swawm iko wapi? Swawm ya huyu haikumfaa. Swawm ya huyu si jengine kwake zaidi ya adhabu. Amejizuia yeye mwenyewe kula na kunywa, lakini hata hivyo hakufanya uhakika wa swawm kama inavyotakikana.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 02
  • Imechapishwa: 23/09/2020