Ibn ´Uthaymiyn kuhusu utumiaji wa dawa zinazomlewesha mgonjwa

Swali: Madawa mengi yaliyoko kwenye maduka ya madawa yana asilimia fulani ya alcohol. Wakati fulani inaweza kuwa vigumu mtu kuziepuka kwa sababu ya kule watu kuzihitajia. Ni ipi hukumu ya kuzitumia?

Jibu: Hukumu ya kuzitumia ni kwamba ikiwa hiki kidogo kilichochangwa na alcohol katika dawa hii hakiathiri. Bi maana kwa msemo mwingine hakina taathira yoyote pale ambapo mtu atakitumia hakitomlewesha, ijapokuwa atatumia sehemu yake kubwa, katika hali hiyo haidhuru. Kwa sababu alchol iliyomo ndani haikuleta taathira yoyote.

Ama ikiwa alchol hii ina asilimia kubwa kwa njia ya kwamba mtu akitumia dawa hiyo kidogo au sehemu yake kubwa itamlewesha. Basi katika hali hiyo itakuwa haijuzu. Ni wajibu kubadilisha dawa hizo kwa dawa zengine ambazo zimesalimika na mambo hayo. Nimefikiwa na khabari kwamba hii leo wamefikia katika kujitosheleza na dawa hizi za alcohol kwa kutumia madawa mengine. Huenda dawa hizo zikawa nyingi – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.sahab.net/forums/index.php?app=forums&module=forums&controller=topic&id=134339