80- Ni lazima kwa mahujaji wote kuswali Fajr Muzdalifah isipokuwa wadhaifu na wanawake. Inafaa kwa wadhaifu na wanawake kuondoka mahali hapo baada ya nusu ya usiku kwa sababu ya kuepuka msongamano wa watu.

81- Kisha ataenda katika al-Mash´ar al-Haraam – nao ni mlima ulioko Muzdalifah. Mtu atapofika hapo, apanda juu yake na aelekee Qiblah na kusema “Alhamdulillaah”, “Allaahu Akbar”, “Laa ilaaha illa Allaah”, ampwekeshe na kumuomba na aendelee katika hali hiyo mpaka kupambazuke kisawasawa.

82- Muzdalifah kote ni mahali pa kusimama. Popote ataposimama mtu itafaa.

83- Kisha aondoke kabla ya jua kuchomoza kuelekea Minaa kwa utulivu na upole na huku analeta Talbiyah.

84- Atapofika kwenye bonde la Muhassir, basi atembee kwa haraka akiweza. Sehemu hii ni katika Minaa.

85- Kisha ashike njia ya kati na kati ambayo itamwelekeza yeye katika nguzo kubwa ya kutupa mawe (al-Jamrah al-Kubra).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 31
  • Imechapishwa: 17/07/2018