Swali: Ni maoni yepi yaliyo na nguvu juu ya swalah ya anayeswali peke yake nyuma ya safu asipopata atayepanga naye safu na akawa anayepanga naye safu ni mtoto wa kiume mdogo na khaswa pindi atapomdiriki imamu ilihali amerukuu?
Jibu: Maoni yenye nguvu ni kwamba mtu asipopata sehemu katika safu basi apange safu peke yake na wala hakuna neno. Hilo ni kutokana na maneno Yake (Tabaarak wa Ta´ala):
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]
Huyu hawezi. Isipokuwa kwa kitu ambacho kina madhara. Kitu chenye madhara ni ima amvute mtu kutoka katika safu, jambo ambalo ni kosa. Huku ni kumtumia mtu pasi na idhini yake. Jengine ni kwamba amemfanyia vibaya mtu huyu kwa kumtoa sehemu bora na kumpeleka sehemu yenye kushindwa ubora. Jengine tena amefungua upenyo. Sababu nyingine ni kuwa hilo litapelekea safu yote kutikisika na wamoja kusogea karibu na wengine. Hapa ni pale ambapo tutasema kuwa mmoja arudi nyuma na kumuunga. Tukisema aende kusimama na imamu, hili pia lina madhara. Akisimama na imamu ameenda kinyume na Sunnah. Sunnah ni imamu asimame sehemu peke yake na si kusimama na mtu. Tukisema kwamba aingie pamoja na imamu hilo litapelekea safu kukatika. Safu nyingi zinakatika kwa kiasi cha wale walioko pale; inaweza kuwa safu moja, mbili, tatu, nne au zaidi ya hapo. Hilo likawa na madhara. Vilevile endapo tutasema aende kupanga safu karibu na imamu halafu baada ya hapo akaja mtu na safu ikawa imekamilika, itambidi huyu pia ende kule kwa imamu na hapo watakuwa watatu. Baadaye akaja mwingine wa tatu na akakuta safu imekamilika, itambidi huyu pia aende kwa imamu na hapo watakuwa wane na huenda wakatimiza safu kamilifu. Upande mwingine endapo atapanga safu mwenyewe nyuma ya safu na akaja mwingine wakapanga naye safu hiyo tayari itakuwa ni safu.
Swali kwamba inafaa kusimama na mtoto? Tunasema ndio. Inafaa kwake kusimama na mtoto. Inafaa kwa mtoto kupanga safu na aliyebaleghe na hakuna ubaya. Anas bin Maalik alipanga safu pamoja na yatima mmoja nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtu anaweza kuuliza kwa kuhoji kama swalah ya mtoto huyu inasihi. Jibu ni ndio. Kila ambaye swalah yake inasihi, inasihi vilevile kupanga naye safu. Isipokuwa tu mwanamke pamoja na mwanamume. Kila ambaye inasihi kupanga naye safu uimamu wake pia unasihi. Kwa ajili hiyo imethibiti kwamba kuna kundi la watu lilimjia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akasema:
“Awaongozeni yule ambaye ana Qur-aan nyingi katika nyinyi.”
´Amr bin Salamah al-Jarmiy ndiye ambaye alikuwa na sehemu kubwa ya Qur-aan na yeye ndiye wakamfanya kuwa imamu. Alikuwa na ima miaka sita au saba. Yeye ndiye walimfanya imamu wa kabila lote katika swalah za faradhi. Hakuwa isipokuwa na miaka na ima miaka sita au saba. Hivi ndivyo ilivyokuja katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy.
[1] 64:16
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/838
- Imechapishwa: 10/06/2020

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/838
Imechapishwa: 10/06/2020
https://firqatunnajia.com/ibn-uthaymiyn-kuhusu-mtu-kupanga-safu-peke-yake-nyuma-ya-safu/